Waziri asisitiza juu ya suala zima la kufanya kazi kwa uwazi ili kuleta tija katika mifumo mbali mbali ya kiserikali

Mhe. Waziri amesisita juu ya suala zima la kufanya kazi kwa uwazi ili kuleta tija katika mifumo mbali mbali ya kiserikali hususan katika suala zima la ukusanyaji wa mapato, ulinzi na uhifadhi wa taarifa muhimu za mitandao.

Nae Katibu Mkuu OFISI YA RAIS IKULU ndugu SALEH JUMA MUSSA amesisitiza juu ya suala zima la uzalendo kwa wafanyakazi, heshima baina ya wafanyakazi na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku.

Vile vile, ndugu SAID SEIF SAID – Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao amewashukuru viongozi hao wa OFISI YA RAIS IKULU kwa kufika katika ofisi ya Mamlaka kwa ajili ya kuzungumza na wafanyakazi na kuahidi kuyafanyia kazi yale yote aliyowaeleza.