Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Zanzibar, Mhe Ali Suleiman Ameir amefanya kikao na viongozi na watumishi wa Mamlaka ya Serikali Mtandao

WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS IKULU – ZANZIBAR

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Zanzibar, Mhe Ali Suleiman Ameir amefanya kikao na viongozi na watumishi wa Mamlaka ya Serikali Mtandao leo tarehe 31.07.2024 Mazizini Zanzibar.

Lengo la kikao hicho ni kujitambulisha rasmi kwa viongozi na wafanyakazi hao baada ya Mamlaka hiyo kuhamishwa kutoka WIZARA YA KATIBA, SHERIA, UTUMISHI NA UTAWALA BORA na kuja katika usimamizi wa OFISI YA RAIS IKULU.

Mhe. Waziri amewataka wafanyakazi wa Mamlaka hiyo kuendeleza yale mazuri yaliyokuwa yakifanyika kabla ya kuhamia OFISI YA RAIS IKULU pamoja na kuboresha sehemu ambazo zilikua na changamoto za kiutendaji.

Amesema kuwa Serikali ina mategemeo makubwa kutoka kwa Mamlaka hiyo, hivyo wafanyakazi wa Mamlaka watumie weledi wao katika kufikia malengo ya Serikali.