Intaneti Serikalini

Wakala wa Serikali Mtandao, inatoa huduma ya mtandao kwa taasisi nyengine za serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Huduma hii inapatikana kwa taasisi za serikali ambazo zimeshaunganishwa kwenye mkonga wa mawasiliano. Taasisi yoyote ya serikali inayo haki ya kutumia huduma hii mara tu baada ya kuwasiliana na Wakala wetu, na kukamilisha ununuzi wa vifaa vinavohitajika ambavyo vitatumika kupokea huduma hiyo. Wakala wa Serikali Mtandao inaendelea kuimarisha huduma hii, ili iwe bora zaidi na kupatikana kwa kasi ya uhakika.

Wakala ya serikali mtandao kwa kushirikiana na wizara ya mawasiliano, inaendelea kuziunganisha taasisi za serikali, Unguja na Pemba ili ziweze kufaidika na huduma hii, mpaka sasa ni zaidi ya taasisi 100 zimeshaunganishwa na zinatumia huduma hii kwa kazi za kila siku. Taasisi yoyote ambayo inahitaji kupata huduma hii, inashauriwa kuwasiliana na Wakala wa Serikali Mtandao, kwa kutumia anuani zinaoonekana kwenye tovuti hii. Kwa hatua za awali, taasisi husika inaombwa iwe na mfumo wa ndani wa mawasilinao, yaani LAN ili iwe rahisi kwa hatua zozote zitazofuata ili waweze kupatiwa huduma hii.