Kuhifadhi Tovuti za Serikali

Wakala wa Serikali Mtandao, imejiimarisha katika kuhakikisha usalama wa tovuti serikalini unakua ni kipaumbele cha kwanza, hivyo wakala serikali mtandao, imetengeneza mfumo wa kisasa ambao utawezesha tovuti za serikali kuhifadhiwa kwa pamoja na kwa usalama zaidi. Taasisi zote za serikali ambazo zimehifadhi tovuti zake nje, zinaombwa kufata utaratibu na muongozo ambao wakala imeshatoa, jinsi gani ya kupata huduma hii kwa kutumia mfumo uliopo wa kuhifadhia tovuti hizo ambao unamilikiwa na Wakala wa Serikali mtandao. Kwa maelezo zaidi usisite kuwasiliana na wakala kupitia anuani zake zilizopo kwenye tovuti hii.