Mamlaka ya Serikali Mtandao Zanzibar (eGAZ) imeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Mamlaka ya Serikali Mtandao Zanzibar Na. 1 ya Mwaka 2024, ikiwa taasisi huru ya umma chini ya Ofisi ya Rais, inayosimamia masuala ya TEHAMA na Serikali Mtandao.
Muundo wa eGAZ unajumuisha vitengo na idara kuu zifuatazo:
- Bodi ya Wakurugenzi
- Chombo cha juu cha kutoa mwelekeo wa kimkakati na kusimamia utendaji wa Mamlaka.
- Inahakikisha uwajibikaji, uwazi na ufanisi wa eGAZ.
- Mkurugenzi Mkuu
- Mtendaji Mkuu wa Mamlaka, anayeongoza shughuli za kila siku.
- Anawajibika kwa utekelezaji wa sera, mipango, na mikakati ya eGAZ.
- Idara Kuu za Mamlaka ya Serikali Mtandao
- Idara ya Usimamizi wa Miundombinu na Mifumo ya TEHAMA
- Kusimamia na kuendeleza miundombinu ya TEHAMA ya Serikali pamoja (mitandao, vituo vya data, n.k).
- Kuhakikisha usalama na uimara wa huduma za kidijitali.
- Kuratibu na kusimamia maendeleo, utekelezaji na uunganishaji wa mifumo ya Serikali Mtandao.
- Idara ya Huduma za TEHAMA kwa Taasisi za Serikali
- Kutoa huduma za ushauri wa kitaalamu wa TEHAMA kwa taasisi za serikali.
- Kur atibu uunganishaji wa huduma za TEHAMA serikalini.
- Kutoa miongozo ya viwango na usalama wa mifumo.
- Kuandaa sera, mikakati, miongozo na tafiti kuhusu matumizi ya TEHAMA katika sekta ya umma.
- Kufanya tathmini na ufuatiliaji wa utekelezaji wa programu za TEHAMA.
- Idara ya Utumishi, Mipango na Rasilimali
- Kusimamia rasilimali watu, fedha, manunuzi, na huduma nyingine za kiutawala.
- Idara ya Usimamizi wa Miundombinu na Mifumo ya TEHAMA