Kwa mujibu wa Sheria Na. 1 ya Mwaka 2024, majukumu ya eGAZ ni pamoja na:
- Kuratibu utekelezaji wa Serikali Mtandao Zanzibar, ikiwa ni pamoja na uundaji wa sera, viwango, na miongozo ya TEHAMA serikalini.
- Kusimamia na kuendeleza miundombinu ya TEHAMA ya Serikali, kama vile Data Center, Mtandao wa Serikali, huduma za usalama mtandao, nk.
- Kutoa huduma za pamoja (shared services) kwa taasisi za serikali kama mfumo wa barua pepe rasmi, mifumo ya malipo, hifadhi ya taarifa, nk.
- Kuhakikisha usalama wa taarifa za serikali kwa njia ya kidijitali, kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama wa kimtandao.
- Kutoa mafunzo, ushauri wa kitaalamu na kujenga uwezo kwa taasisi za serikali kuhusu matumizi sahihi ya TEHAMA.
- Kufanya tafiti, tathmini na kutoa mapendekezo ya kisera na kiufundi kuhusu matumizi ya teknolojia katika sekta ya umma.
- Kuhamasisha matumizi ya TEHAMA kwa wananchi, ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za serikali kwa njia ya mtandao.
- Kusimamia maendeleo ya mifumo ya kitaifa ya TEHAMA, kama mifumo ya usajili, malipo, afya, elimu, biashara, utalii, nk.
- Kuratibu ushirikiano wa kimataifa na mashirika ya maendeleo katika nyanja za TEHAMA na Serikali Mtandao.