- info@egaz.go.tz
- wasiliana Nasi
- FAQ
Menu
Utafiti umeonesha kwamba baadhi ya Taasisi za Umma BADO zinapokea pesa Taslimu (Cash) na nyengine zinatengeneza “Control Number” ambazo hazifahamiki na ZanMalipo katika utowaji wa huduma. Kufanya hivyo ni kosa kisheria.
Kwa mujibu wa Kifungu Namba 55A cha marekebisho ya mwaka 2021, ya Sheria ya Usimamizi wa fedha za Umma namba 12 ya mwaka 2016, Fedha zote za Umma zinatakiwa kukusanywa kupitia mfumo wa Malipo ya Kielektroniki wa ZanMalipo. Taasisi za Umma kufanya kinyume na utaratibu huo. Ni Kuvunja Sheria za Nchi.