Wakala ina majukumu yafuatayo:
- kuandaa na kusimamia utekelezaji wa sera za TEHAMA, kanuni na miongozo katika utumishl wa umma;
- kusimamia maendeleo na matumizi ya TEHAMA katika utumishi wa umma;
- kutekeleza maagizo ya kisera na maamuzi mengine ya Serikali kuhusiana na matumizi ya TEHAMA katika utumishi wa umma;
- kuanzisha mifumo ya utekelezaji kwa ajili ya kuwezesha na kuratibu upatikanaji huduma za serikali mtandao
- kushauri mamlaka husika na taasisi yoyote ya umma juu ya matumizi bora ya TEHAMA katika usimamizi na utoaji wa huduma za umma;
- kuanzisha, kusimamia na kuendeleza mifumo ya pamoja ya serikali mtandao na huduma;
- kuanzisha na kuendeleza mifumo ya taarifa huru kwa ajili ya matumizi ya umma;
- kuoanisha, kuratibu na kuendeleza shughuli za serikali mtandao katika taasisi za umma;
- kuanzisha na kuendeleza rejista za mifumo ya serikali mtandao na huduma;
- kuandaa na kuweka kumbukumbu za wataalamu wa TEHAMA kupendekeza maslahi na kuratibu matumizi ya wataalamu hao katika utumishi wa umma;
- kusimamia miradi ya serikali mtandao inayotekelezwa na taasisi za umma;
- kuanzisha mfumo wa ufuatiliaji na tathmini kwa ajili ya kutathmini utendaji kazi wa Serikali Mtandao;
- kuthibitisha mifumo ya taarifa inaendana na mahitaji ya mifumo mingine na usalama;
- kutumia uwezo Chini ya mikataba na makubaliano yaliyokubaliwa na Serikali kuhusiana na masuala ya Serikali Mtandao;
- kufanya taflti na kazi za kimaendeleo kuhusiana na masuala ya serikali mtandao; na
- kutekeleza kazi nyengine yoyote ambayo ni muhimu kwa ajili ya utekelezaji wa malengo yake Chini ya Sheria hii.