Wakala wa Serikali Mtandao ni taasisi ya Umma iliyoanzishwa kupitia sheria nambari 12 ya mwaka 2019 yenye jukumu la kuratibu, kusimamia na kukuza jitihada za Serikali Mtandao pamoja na kuhimiza utekelezaji wa Sera, Sheria, Kanuni, Viwango na Miongozo ya Serikali Mtandao kwa taasisi za umma.
Dira
Kuwa kitovu cha utaalamu na ubunifu chenye kurahisisha upatikanaji wa huduma za TEHAMA serikalini
Dhamira
- Kutoa huduma bora kwa umma na kukuza utawala bora kwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano iliyo salama na yenye kuaminika.
Malengo:
- Kuratibu shughuli za serikali mtandao kwenye taasisi za umma na utoaji huduma kupitia matumizi ya TEHAMA.
- kuhakikisha mifumo ya habari na mawasiliano inawekwa, inaimarishwa na inaendelezwa kwa mujibu wa sera na viwango itakayopelekea kuwa na upashanaji habari mzuri, wenye gharama nafuu utakaorahisisha shughuli za Serikali;
- kuhakikisha upatikanaji wa huduma za Serikali nchi nzima kwa urahisi. ufanisi, uthabiti, kwa kutumia mifumo sahihi ya TEHAMA;
- kushajihisha matumizi ya TEHAMA katika utumishi wa umma; na
- kuwa kitovu cha utaalamu katika kuandaa na kuendeleza sera, viwango na taratibu nyengine kwa ajili ya kuimarisba matumizi ya TEHAMA katika utumishi wa umma Zanzibar.