- info@egaz.go.tz
- wasiliana Nasi
- Maswali
Menu
Mwanzo » Maswali
Ni mabadiliko ya utoaji huduma za Serikali kwa ufanisi,urahisi na uwazi kwa raia /wananchi na wafanyabiashara kwa kutumia TEknolojia ya HAbari na MAwasiliano (TEHAMA)
Wakala wa Mkonga na miundombinu ya TEHAMA ni taasisi inayosimamia na kusambaza miundombinu ya TEHAMA serikalini pamoja na kusimamia kituo kikuu cha kuhifadhia taarifa (Data Center).
Wakala wa Serikali Mtandao ni taasisi inayosimamia Huduma za TEHAMA serikalini ikiwemo kutoa miongozo, sera na kanuni, utengenezaji wa mifumo , usimamizi wa miradi, ununuzi wa vifaa, huduma za kimtandao pamoja na kutoa ushauri wa kitaalamu juu ya matumizi ya TEHAMA.
Barua pepe ya Serikali ni barua pepe maalumu inayotengenezwa kwa anuani maalum za Serikali kwa ajili ya kusaidia mawasiliano ya kikazi ya kila siku kwa watumishi wa Umma.
Kupata barua pepe ya Serikali, Mtumishi anatakiwa kuandika barua kwa Wakala wa Serikali Mtandao kuomba kutengenezewa barua pepe na hatua nyengine zitafuata.
Nyaraka za mifumo zilizomo ndani ya tovuti zitatumika kulingana na mahitaji.
Nyaraka zote zinatakiwa zijazwe kulingana na maelezo yaliyomo, zisainiwe na wahusika na ziwasilishwe Wakala wa Serikali Mtandao kwa ajili ya kuidhinishwa.Ili kupata nyaraka hizi bonyeza anuani hii Mwanzo/Nyaraka.
© 2025 - eGAZ. Haki zote zimehifadhiwa
Imetayarishwa na Kusanifiwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao Zanzibar