Wakala wa Serikali Mtandao imetayarisha na kuweka hadharani nyaraka za miongozo na viwango kwa lengo la kusaidia taasisi za umma wakati wa uandaaji na utayarishaji wa mifumo na vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika kuendesha shughuli za taasisi na utoaji wa huduma kielektroniki kwa jamii.
Nyaraka hizi zinatoa muongozo kwa Wizara, Taasisi, Mamlaka, Serikali za Mitaa na Mashirika yote ya Umma katika manunuzi, uanzishaji, na uendelezaji wa mifumo na vifaa vya TEHAMA ili kuhakikisha manufaa yanayotarajiwa yanapatikana. Kwa maelezo zaidi, tafadhali fungua TOLEO la Manunuzi na Ufungaji wa Mifumo na Vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasilino (TEHAMA) katika sekta ya Umma.